SECURITY YA SIM YAKO NI MUHIMU SOMA.

  
Hello na karibu tena katika muendelezo wa mafunzo murua ya technology. Baada ya kuchunguza kwa mda sasa nimetambua watu wengi huishia kulia baada ya kupoteza sim zao au kujiridhisha kwa kublock namba aliokua anatumia. THAT IS NOT (NOT,NOT,NOT) THE SOLUTION.  Kuna mambo ya haraka na muhim ya kufanya imidietly sim yako inapopotea lakini muhim mambo ya kufanya kabla sim haijapotea.
YAFUATAYO NI MAMBO MUHIM YA KUFANYA KABLA YA KUPOTEZA SIM
1)PASSWORD

  Kumbuka hapa siongelei passcode ama pattern naongelea password haswa. Ili password iwe protective inatakiwa iwe na 8 ama zaid ya 8 characters. Kwa watu wanaoelewa password zao huwa mchanganyiko na sio kitu kirahi kuguess.
Kwa mfano "lilian1995" hio ni password rahisi mtu anaweza kuguess very simple.
But password kama "!ohn5991" inakua ngumu kidogo hata wewe owner .
Nafurahishwa na technology ya sasa ya biometric kweli inaplay part kubwa katika security
2) TUMIA "FIND MY PHONE" app
      Hizi app ziko nyingi na unaweza kuzidownload playstore na app store for free. My advice tumia ile iliokuja na software ya sim yako. Kama ni android tumia "android device manager " kama ni iphone tumia "find my iphone" na "icloud" kama ni blackberry tumia "blackberry pocket".
3) note down code special ya sim yako (imei)
       Hii inatambulika kwa kudial *06# hii hua very unique na special for your phone only. Hii unaweza kuitumia hata wakati unareport upotevu wa sim yako.  Kumbuka imei ni kitu kama id keep it to your self. Naona mitandaoni watu wanakuomba imei ili wakufungulie, dont do it it will cost you.
YAFUATAYO NI MAMBO MUHIM YA KUFANYA BAADA YA KUPOTEZA SIM YAKO
1)wahi haraka katika computer ya karibu yenye internet na jaribu kutrac sim yako. Kama iko mbali na wewe na unaona kama itachukua mda kuifikia hit erase. Hii itafuta data za sim and if yua lucky kama unatumia iphone that will be the end of it.
2) pale unapotambua tu sim haipo mikononi mwako cha kufanya ni kujaribu kubadili password zako muhim. Kama GMail na app nyingine za umuhim. Hii itasaidi kuzua mualifu kupata persona information
3) Fahamisha institution muhim zeney details zako kuhusu upotevu huu. Hii itasaidia kuepuka kua frouded.
4) Ripoti kesi hii polisi kwa upelelezi zaidi. Wakati huopia jitahifi ue umeshablok namba yako ya sim.
FANYA HAYA BAADA YA KUPATA SIM YAKO
   Mara nyingi watu wakipata sim zao huishia kuanza kufurahi na kutumia. Hujui aliekua na sim yako aliweka nini huko ndani. So cha kufanya ukishaipata sim ni kuifuta kila kitu kwa kutumia hard reset .
Huu sio mwisho bali mwendelezo wa article nyingi za nguvu karibuni.

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU NA ZITAMBUE TOFAUTI KATI YA IPHONE ORIGINAL NA CLONE

ONGEZA KASI YA PC YAKO

IFAHAMU SIM YA TECNO C8