ONGEZA KASI YA PC YAKO
Leo tutatizama njia za kuifanya computer yako ifanye kazi kwa kasi na kupunguza matatizo ya hapa na pale. Hii ni maalumu kwako kama unatumia platform yoyote ya Windows, iwe Windows 7, 8 au 8.1. Haijalishi kama computer yako ni ya bei ghali sana, ina processor na RAM kubwa lakini kama utendaji kazi wake ni wa kusuasua haina maana sana.
Labda computer yako huchelewa sana kuwaka au kufungua mafaili. Au inaganda na kujiwasha upya pasipo sababu ya msingi unayoifahamu. Usihofu, mambo yafuatayo ni muhimu kwako kama unaijali computer yako. Unaweza pia kusoma computer bora kwa ajili yako na laptop bora za mwaka 2014.
Nimeandaa hii kwa kuunganisha Windows 7 na 8, Windows 8 haina Start button hivyo tumia sana sehemu ya Search pembeni mwa screen yako.
- ZUIA PROGRAMU ZINAZOFUNGUKA PINDI UNAPOWASHA COMPUTER.

- BONYEZA kwenye keyboard vitufe hivi kwa wakati mmoja Ctrl + Shift + Esc.
- Subiri kidogo baada ya muda itafunguka Task Manager. Angalia katika vipengele vyake na chagua sehemu iliyoandikwa Start Up.Hapo utaona list ya program zote zinazofunguka punde unapowasha computer yako. Utaweza kuona uzito wake kuna None. Low, Medium na High.
- Zuia program usizozihitaji hasa zitakazo kuwa na Medium na High.
- TUMIA PERFORMANCE TROUBLESHOOTER YA WINDOWS.
Microsoft wakati wanatengeneza window hujua kabisa kwamba matatizo yatatokea. Na saa nyingine matatizo ambayo hayagunduliki kwa urahisi na mtumiaji. Hivyo katika computer yako kuna program ya Performance Troubleshooter. Hii hutafuta na kurekebisha matatizo mengi katika utendaji kazi wa computer yako automatically. Ili kuitumia Performance Troubleshooter;
- FUNGUA> Control Panel (Windows 7 inapatikana kupitia Start, Windows 8 elekeza mshale wa kipanya katika upande wa chini kuchoto kisha Right Click sio Left Click unaweza Search - Control Panel)
- Ukishafungua Control Panel, andika Troubleshooter katika search box.
- Kisha bonyeza Troubleshooting
- Chini ya System and Security mwishoni bofya Check for Performance Issues (Windows 8 chagua Run Maintainance Tasks).
- SAFISHA COMPUTER YAKO KWA CCLEANER
Nimewahi kuzungumzia CCleaner katika post yangu ya Programu 10 za muhimu kwa ajili ya computer, hii programu ni nzuri sana katika kutunza computer yako. Ni ya bure ingawa baadhi ya huduma zake za advanced unaweza kuhitajika kulipia. Bure ni nzuri pia. Tumia hii kusafisha computer yako na pia kusafisha Registry. Pia unaweza kutumia kufuta sehemu zisizokuwa na kitu (kama mapengo) katika hard disk. Download CCleaner hapa.
- FUNGUA PROGRAMU CHACHE KWA WAKATI MMOJA
- RESTART COMPUTER MARA KWA MARA.
Hii itasaidia kutumia RAM yako vizuri. Unapowasha computer yako data zote zinatunzwa katika RAM. Hivyo ukitumia computer kwa muda mrefu mambo mengi yatachukua nafasi katika RAM yako. Unapozima computer RAM hufuta data zote na ukiiwasha RAM huwa safi na kuweza kutumika tena. Lakini pia computer ina tabia ya kupata joto sana. Joto sio rafiki mzuri wa kifaa chochote cha chuma hivyo ukiizima na kuiwasha kidogo inapoa.
- ZIMA BAADHI YA VISUAL EFFECTS.
Tulia. Usichanganikiwe na mambo. Hapa panahitaji umakini wako kidogo. Visual Effects hizi ndizo zinaifanya windows iwe na muonekano fulani. Visual Effects huipa windows muonekano wa kuvutia. Lakini hizi hunyonya nguvu nyingi ya computer pia. Hivyo ninakushauri kutumia njia hii kama computer yako imeelemewa sana na shughuli. Ili kuzima baadhi ya Visual effects;
- FUNGUA - Control Panel
- Kisha search Performance Information and Tools. Kisha katika list chagua tena Performance Information and Tools. (Windows 8, unaweza kusearch moja kwa moja Performance Information and Tools kupitia Search kulia mwa screen yako, chagua Settings kupata majibu).
- Bonyeza Adjust Visual Effects, ingiza password yako administrator kama ikihitajika.
- Bonyeza kipengele cha Visual Effects, bofya Adjust for Best performancekisha bonyeza OK. Kama wewe sio mtaalamu sana hapa chagua tu Let windows choose what's best for my computer. Kisha Bofya OK.

Shukrani kwa kuendelea kutembelea blogu yetu hii. Ukipata tatizo lolote usisite kunitumia ujumbe. Maoni na ushauri yanakaribishwa pia.
Comments