FAHAMU NA ZITAMBUE TOFAUTI KATI YA IPHONE ORIGINAL NA CLONE

FAHAMU NA ZITAMBUE TOFAUTI KATI YA IPHONE ORIGINAL NA CLONE

IPhone ni moja ya gadgets maarufu katika soko. Hii imethibitishwa na mauzo kuongezeka na pia ubora wa bidhaa kua maintained. pia IPhone inazidi kua maarufu kutokana na perfomance na pia heshma anayopata mtumiaji wa sim hii. Apple wameitengeneza iphone ikiambatana na several apps ambazo zitakusaidia on your daily basis. IPhone mpya kawaida gharama karibu $ 699. inaweza kuonekana kidogo ghali, lakini watu wengi huamini kuwa  thamani ya fedha na bidhaa wanayopata vinaendana. Kutokana na hili basi hata wazalishaji wa sim fake kutumia mgongo wa Apple kupitisha bidhaa zao sokoni.

hapa leo utajifunza tofauti kati ya ile fake na original. Wazalishaji wa sim hizi bandia hujitahidi sana kufanya bidhaa yao kua sawa na ile ya halali ili tuu kumchanganya mnunuzi.Ni ngumu kuwazuia wazalishaji hawa kuacha kuingiza bidhaa zao sokoni. Nini kifanyike ni kuelimisha watu ili kupunguza kuongezeka kwa idadi ya wanaotapeliwa. Kwa wale ambao wanataka kununua iPhone kwa mara ya kwanza, huu utakuwa mwongozo mzuri kwa ajili yenu kutofautisha  iPhone kati ya original na cloned. Kama wewe ni mpenzi wa iPhone, bado unaweza kushare chapisho hili pamoja na familia au marafiki , ili nao kujua kutofautisha kati ya iphone fake na original. Ni bora kuanza na sifa za maumbile na kuhusu program na perfomance yatafuta next time.

JINSI YA KUTAMBUA KAMA IPHONE YAKO NI ORIGINAL
  1. Angalia screws.    IPhone original hutumia screw za  pentalobe, wakati clone  anatumia screws kawaida msalaba.Apple amefanya ivo ili iwe rahisi kutofautisha bidhaa zake na za bandia. 
  2. Angalia eneo la button. jinsi nyingine ya kutambua iphone original na fake ni kwa kuangalia mpangilio wa button. katika original button ya kueka silent na za sauti huwa juu upande wa kushoto. Ila fake nyingi huwa upande wa kulia.
  3. Angalia memory capacity Iphone original inakua na fixed memory 16GB, 32GB, 64GB na 128GB. ila fake lazima watumie external memmory ili kuexpand.hivo basi ukiangalia na ukakuta slot ya memory card jua hio ni fake.
Kwa leo naomba tuishie hapo ila next time tutazungumzia kuifahamu kwa kuiwasha na kuangalia other features asanteni.

  1. Tazama welcome screen zima sim kisha washa na tazama log in screen. Fake nyini huonyesha logo ya Android ama maneno kama welcome, wakati original yenyewe huonyesha logo ya Apple. Pia jaribu kuangalia katika home screen na ufungue app ya AppStore ikikupeleka playstore basi tambua ni fake.
  2. Cheki Application ya Siri Hii ni App ambayo iDevices tuu ndo zina uwezo wa kusoma na kuirun. hivo kama si original itashindwa kabisa.
  3. Tazama Operating Systeam Kama utaona kitu chochote tofauti na iOSbasi jua hio sim ni feki kabisaa. iPhone inatumia iOS tuu na si vinginevo
  4. Unganisha kwenye iTunes Unganisha sim yako na kompyuta yako kupitia waya na fungua app ya iTunes kwenye Laptop/Pc yako. kama haitasoma sim ako basi jua tayari ni fake
Asanteni sana na hapa tumefika mwisho wa muendelezo wetu wa jinsi ya kutambua iPhone ya halali na Fake one. Tembelea ukurasa huu mara kwa mara kujionea machapisho mapya. pale ambapo unakwama uliza kwenye comment box au tuandikie barua pepe kupitia techedutanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

ONGEZA KASI YA PC YAKO

IFAHAMU SIM YA TECNO C8