KABLA YA KUNUNUA SAMSUNG GALAXY FANYA HAYA
Wengi wetu tumekua tukipenda kununua sim mikononi mwa watu {second hand} kutokana na unafuu wa bei. ila kumekua na ulaghai na utapeli hasa kwa wale wasiojua kutofautisha kati ya sim original na fake. Leo nitazungumzia sana sim za samsung, kwani ndio zimerindima humo mitaani mwetu.
Simu za Samsung Galaxy ni moja ya simu maarufu katika soko. Kila mwaka, kampuni ya samsung hutoa bidhaa mpya ya Galaxy, ambayo kwa kifupi huwa ni bora na muendelezo wa toleo lililopita. Hii ni moja ya sababu inayopelekea wazalishaji wa sim fake {cloned } kutumia mwanya huo kuingiza sim zao sokoni. Tofauti na iphone kwa kutumia iOS programu ya Apple ambao wao pekee ndo licensed owner , Simu za Samsung Galaxy hutumia Google open source ya Android na kuifanya rahisi na nafuu kwa wazalishaji wa clone na feki.
JINSI YA KUTAMBUA GALAXY FAKE NA ORIGINAL
Je umewahi kununua Samsung Galaxy Note 3/4/5 na sasa unahisi ni fake kwa sababu ya performance ndogo? Je? umeona mahali simu ya samsung inauzwa kwa bei rahisi sana ila unaogopa kununua kwa sababu unahisi ni fake? usipate tabu kwani nitakufahamisha kwa undani zaidi jinsi na namna ya kutambua hilo.
TAMBUA SAMSUNG FAKE KWA KUITAZAMA TUU
Simu nyingi za Clone zinakua zimetengenezwa kwa kutumia material za bei rahisi kutokana na bajeti iliokua imepagwa hasa na watu wa masoko. Hivyo kusaidia kuwa rahisi zaidi kufahamika kwa kuitaza tuu. Yafuatayo ni maeneo au mambo muhimu ya kutazama.
NB: kama huna uzoefu na simu original ni bora kuazima ya rafiki ili unapoenda kununua uziweke zote bega kwa bega na kuzilinganisha.
- SCREEN IMETENGENEZWA KWA KUTUMIA CHEAP GLASS MATERIAL {kwa kutumia kiganja chako jaribu kurub screen zote mbili na kuskizia tofauti moja huwa rough na ingine smooth}
- SCREEN IKO MBALI SANA NA UKINGO {EDGE } ZA SIMU
- LOGO YA SAMSUNG HAIJAWA SMOOTHED NA UNAWEZA KABISA KUFEEL PALE UNAPORUB
- HOME BUTTON HAIKO KATIKA EXACT POINT INAPOTAKIWA KUWA, HUWA JUU ZAIDI AU CHINI ZAIDI YA ILE YA ORIGINAL
- BAADHI YA SENSOR ZINAKUA HAZIPO
- SCREEN YA FEKI SI BRIGHT NA SMOOTH KAMA YA ORIGINAL
- UKIFUNGUA KWA NYUMA UTAKUTA KUNA VITU VINATOFAUTIANA KWANZIA NATI ZILIZOFUNGIWA MPAKA MAANDISHI NA LOGOZ
- USAWA WA SIMU PIA NI TOFAUTI, MOJA HUWA KUBWA NA NYINGINE NDOGO JAPO KWA millimeter CHACHE SANA {ushauri, unapoenda jaribu kubeba cover ambalo linafiti vizuri kwenye sim original.}
- KWA SIMU KAMA NOTE 3/4/5 TOA KALAMU {S-PEN} NA JARIBU KUTOFAUTISHA {ya fake hua na point ya metal, ya original huwa na pointer ya ruber. Ya fake kuna features haiwezi fanya kama screen grab na pia screen wright.}
Kwa leo tuishie hapo ila nitakuja tena na chapisho lingine kuhusu simu hizihizi ila sasa kwa kutumia mbinu zingine mbalimbali. kama una swali lolote uliza ama tuandikie kupitia techedutanzania@gmail.com
Comments